1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa aingia madarakani

10 Septemba 2025

Waziri Mkuu mpya ni mwenye umri wa miaka 39 ni wa tano nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka miwili. Alikabidhiwa ofisi hii leo na Waziri Mkuu anayeondoka Francois Bayrou.

Paris I  2025 | Sebastien Lecornu
Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu Picha: Gao Jing/Xinhua/picture alliance

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu ameingia madarakani huku kukiwa na maandamano katika jiji la Paris ambayo yametatiza shughuli za usafiri, elimu na huduma nyinginezo.

Maandamano hayo yanafanyika kuonyesha hasira ya umma dhidi ya hatua za Rais Emmanuel Macron. Takriban askari elfu 80 wametawanywa marabarani na watu kadhaa wamekamatwa hadi kufikia sasa.

Waziri Mkuu mpya ni mwenye umri wa miaka 39 ni wa tano nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka miwili. Alikabidhiwa ofisi hii leo na Waziri Mkuu anayeondoka Francois Bayrou, ambaye serikali yake iliangushwa baada ya kushindwa katika kura ya imani Bungeni.

Sebastien Lecornu ameahidi kubuni njia za kufanya kazi kwa pamoja na wapinzani katika kuidhinisha bajeti itakayopunguza deni la taifa na pia kuzipitia upya sera za serikali.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW