SiasaUfaransa
Bayrou anusurika na kura ya kutokuwa na imani Bungeni
17 Januari 2025Matangazo
Bayrou amenusurika na kura hiyo baada ya vyama vya mrengo wa kulia na mrengo wa kati kukataa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na chama cha mrengo wa kushoto cha La France Insoumise (LFI).
Chama hicho kinachoongozwa na Jean-Luc Melenchon kiliitisha kura hiyo baada ya Bayrou kupendekeza kuanzishwa tena kwa mazungumzo kuhusu mageuzi ya mfumo wa pensheni yenye lengo la kusaidia kupunguza nakisi iliyokithiri katika bajeti ya mwaka huu.
Ufaransa ilikabiliwa na mzozo wa kisiasa mwaka jana wakati Macron alipoitisha uchaguzi wa mapema wa Bunge ambao matokeo yake yamesababisha kuwepo mkwamo mkubwa kutokana na kwamba hakuna chama chenye wingi wa kutosha bungeni.