1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu mpya wa Ufaransa atangaza mpango wa serekali yake

9 Juni 2005

Waziri mkuu mpya wa Ufaransa, Dominique de Villepin, ametangaza kwamba mapambano dhidi ya ukosefu wa kazi ndilo suala muhimu litakaloishughulisha serekali yake. Katika taarifa ya mwanzo ya serekali yake mbele ya bunge, Bwana de Villepin alitangaza zitatengwa Euro bilioni 4.5 zaidi ili kuunda nafasi za kazi. Kuhusu hatua ya wapigaji kura wa Kifaransa kuikataa katiba ya Ulaya, alisema Wafaransa wameonesha kutostahamili na pia hasira zao. Alisema Wafaransa kuikataa katiba ya Ulaya haina maana kuikataa Ulaya. Wawakilishi wa chama cha upinzani cha kisoshalisti waliyalaumu matamshi hayo ya de Villepin kuwa ni ya kubabisha. Ilivokuwa Wa-Conservative wana wingi bungeni, waziri mkuu huyo mpya alipigiwa kura ya kuwa na imani naye.