Waziri Mkuu Mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu ajiuzulu
6 Oktoba 2025
Ikulu ya Elysée imesema barua ya kujiuzulu ya Lecornu imewasilishwa kwa rais Emmanuel Macron ambaye ameukubali uamuzi huo.
Hatua ya Lecornu kujiuzulu imejiri ikiwa ni saa chache baada ya kuteua baraza lake jipya la mawaziri, ambapo nafasi nyingi muhimu ziliendelea kushikiliwa na mawaziri waliokuwepo. Kabla ya hatua ya Waziri mkuu huyo kujiuzulu, upinzani walitishia kuiangusha serikali yake, jambo linalodhihirisha ni jinsi gani kuna mzozo na mkwamo mkubwa wa kisiasa nchini Ufaransa.
Siasa za Ufaransa ziliingia kwenye misukosuko tangu rais Macron alipochaguliwa tena kwa muhula wa pili mwaka 2022 na zilivurugika kabisa baada ya uchaguzi wa mapema wa Bunge wa mwaka jana ambapo hakuna chama chochote kilichofanikiwa kupata wingi unaohitajika wa wabunge.