Waziri Mkuu Netanyahu anaaza ziara barani Ulaya
4 Juni 2018Uhusiano wa nchi zote mbili unajengeka kutokana na maovu ya kihistoria-mauaji ya wayahudi milioni sita yaliofanywa na utawala wa Wanazi wa Ujerumani. Tangu mwaka 1965, uhusiano umekuwa ukiboreka na huo ndiyo mwaka ambao Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani lilianza uhusiano wa kibalozi na Israel. Upatanishi ulitokana zaidi na David Ben Gurion ( 1886-1973). Licha ya mauaji ya kimbari Waziri mkuu huyo wa kwanza wa Israel aliiona nchi hii kuwa ni Ujerumani nyengine. Ben Gurion na Kansela wa kwanza wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Konrad Adenauer walikutana mara mbili tu- 1960 na 1966- na pamoja na hao viongozi wote wawili walionekana kuwa kama marafiki wa mbali.
Msimamo wa Ujerumani kwa Israel
Leo uhusiano wa nchi hizi ni wa ushirikiano. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Heiko Maas ameueleza uhusiano wa nchi hizi mbili kabla ya ziara yake ya Israel kwa kusema "Ninaamini kwamba takriban sote tunakubaliana kuna tafauti njiani lakini daima Ujerumani itakuwa upande wa Israel katika masuala yote haya.”
Kumbukumbu ya mauaji makubwa ya Wayahudi ni muhimu anasema mwaandishi habari Mjerumani – Muisraili Michael Wolffsohn. Anaipinga ile hoja kwamba mauaji ya kimbari Holocaust ndiyo yaliosababisha kuundwa dola ya Israel: Anasema, " Hilo lazima tulisahihishe. Israel ingekuwepo hata bila ya mauaji ya kimbari na wayahudi milioni sita wangeweza kunusurika.Tofauti za Isra
Tofauti za Israel na Ujerumani
Ujerumani na Israel zinakubaliana mengi. Lakini pia kuna masuala yenye utata hasa panapohusiana na mgogoro wa zaidi ya miaka mia moja kati ya Waisraili na Wapalestina. Zaidi ya hayo baadhi ya vyombo vya habari vingali vikizungumzia uhalali wa kuwepo Israel.Sambamba na hayo ni suala zima la usalama wa dola la Israel.
Waisraili kwa wakati huu wanaangalia kwa hali ya kukerwa, kuwepo kwa hisia za chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani na Ulaya, iwe ni kutoka mrengo wa kushoto, kulia au hata itikali kali za kiislamu. Kwa upande wa Ujerumani Kunakosekana hali ya kuashiria amani kati ya Israel na Wapalestina.Pamoja na yote lakini mshikamano na Israel ni sehemu ya msimamo wa Ujerumani. Katika hotuba yake ya kihistoria mbele ya bunge la Israel-Knesset 2008, Kansela alitoa kauli ya msisimko alipotamka maneno haya " Kila serikali ya Shirikisho na kila Kansela wa Shirikisho aliyenitangulia alijizatiti katika jukumu maalum la kihistoria kwa ajili ya usalama wa Israel."
Kwa muda mrefu ,Ujerumani ni mshirika wa pili muhimu wa kibiashara wa Israel baada ya Marekani na huipatia nyambizi dola la Israel. Kuna miradi kadhaa ya pamoja ya shughuli za utafiti .
Leo hii Ujerumani na Israel zinakubaliana katika mambo mengi.Lakini pia kuna masuala kama ujenzi wa makaazi ya walowezi wakiyahudi. Wengi wa Waisraili wanawashutumu Wajerumani na wengineo barani Ulaya kwa kushindwa kukabiliana ipasavyo na nchi zenye uadui na Israel. Bila shaka uhusiano wa kisiasa haukosi mivutano. Mbali na Ujerumani Netanyahu atazizuru pia Ufaransa na Uingereza.
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/ Knipp,Kersten (DW)
Mhariri:Josephat Charo