SiasaCanada
Waziri Mkuu wa Canada Carney azuru China
14 Januari 2026
Matangazo
Canada inaangazia kuimarisha uhusiano na nchi nyingine, tofauti na Marekani.
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa Canada nchini China katika kipindi cha karibu muongo mmoja. Carney atakutana na Waziri Mkuu Li Qiang pamoja na Rais Xi Jinping.
Carney ameitaja ziara hiyo ya China kama sehemu ya hatua za kujenga ushirika mpya kote ulimwenguni, ili kuhitimisha utegemezi wake kiuchumi kwenye soko la Marekani.
Licha ya Canada kuwa mshirika wa karibu wa Marekani kwa muda mrefu, Rais Donald Trump aliiwekea ushuru mkubwa kwa bidhaa zake zinazouzwa Marekani na kupendekeza kwamba taifa hilo lenye utajiri wa rasilimali linaweza kuwa jimbo la 51 la Marekani.