1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali imewalipa walalamikaji fidia ya dola 50milioni

Admin.WagnerD27 Novemba 2017

Waziri Mkuu wa Canada ameomba radhi kwa watu wa jimbo la Newfoundland na Labrador kutokana na unyanyasaji uliofanywa katika shule za ujuzi wa mabadiliko, zilizokuwa katika mfumo wa bweni miaka 1980.

Justin Trudeau in Neufundland
Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau alipoomba radhi hivi karibuni kwa niaba ya serikali kutokana na unyanyasaji huo uliofanywa miaka ya 80. Picha: picture alliance/AP Photo/A. Vaughan

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau juzi amewaomba radhi watu wa kabila la Newfoundland na wa jimbo la Labrador kutokana na unyanyasaji  uliofanyika katika shule za bweni katika karne  yote ya 20.

``Tupo hapa leo kuomba radhi kutokana na makosa ya kihistoria´´ alisema akiomba radhi kwa unyanyasaji wa kingono, kimwili na kisaikolojia uliofanyika katika shule tano za jimbo hilo.

``Huu ndiyo ukweli mgumu katika historia ya Canada.`` alisema

 Kitendo cha TRUDEAU kuomba radhi kumekuja katika wakati ambapo serikali hiyo imeruhusu kuchukuliwa kwa hatua za kisheria baada ya malalamiko kuletwa  na wanafunzi wa zamani 900 wa shule hizo. Wengi wakiwa ni wale walioondolewa kwa nguvu katika jamii zao na kutengwa na familia zao  katika jitihada ya kulazimishwa kubadilika  na kuingia katika tamaduni zenye wafuasi wengi.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times la Marekani, walalamikaji hao walilipwa  jumla ya dola milioni 50 za Canada kama fidia.

 Katika sherehe hizo, zilizofanyikia  HAPPY VALLEY-GOOSE Bay, pamoja na Trudeau alikuwepo pia Tony Obed, mwanafunzi wa zamani wa shule hizo za bweni , aliyeongoza harakati za  kufunguliwa mashtaka hayo.

 Obed,ambaye alisimulia hadharani  kuhusu unyanyasaji wa kingono aliofanyiwa akiwa shule alikubali hatua ya kuombwa na serikali ya Canada.

Mandhari ya Hifadhi za Milima iliyo katika eneo la Newfoundland na Labrador, Canada.Picha: Imago/All Canada Photos

Mauaji ya kitamaduni

Ni kama mauaji ya utamaduni, kwani mabadiliko hayo ya utamaduni yalifanyika kwa kiasi kikubwa Marekani na Canada katika karne ya 19 na ya 20. Huko Canada baadhi yao  walivumilia hadi mwaka 1996.

Nchini Canada, shule nyingi zilikuwa zikisimamiwa na serikali na wakati mwingine zilisimamiwa na wamishionari au wahisani.

 Wakati Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Stephen Harper alipoomba radhi kwa mitandao ya shule hizo mnamo mwaka 2008, hakuzitaja shule za Newfoundland na Labrador kutokana na kwamba hazikuwa sehemu ya Canada hadi mwaka 1949.

 Tume ya upatanisho na ukweli  iliyoundwa baada ya Harper kuomba radhi, ilibaini kuwa uvunjwaji wa haki  uliofanywa katika shule hizo za bweni ni sawa na mauaji ya kimbari ya tamaduni.

 Utafiti uliofanywa  mwaka 2016 na Wanazuoni wa Kituo cha Mbadala wa Sera cha nchini Canada,  ulibaini kuwa asilimia 60 ya watoto  wenye asili  ya aborigine katika  maeneo ya ndani  nchini humo  wanaishi katika umaskini na kitakwimu, idadi kubwa ya wanawake  ndiyo waliokuwa waathirika wakubwa wa mauaji nchini Canada.

 Mwandishi: Florence Majani

(Mhhttp://www.dw.com/en/trudeau-sorry-for-historic-wrong-against-aboriginal-canadians/a-41527614)

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW