1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiCanada

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akutana na Trump

30 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amekutana na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kufuatia kitisho chake cha kuiongezeea Canada ushuru.

Waziri Mkuu wa canada Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau afanya mazungumzo na Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuangazia ushirikiano wa kiuchumiPicha: Blair Gable/REUTERS

Trudeau amekutana na Trump kwenye makazi yake ya Mar-a-Lago, huko Florida jana Ijumaa.

Mkutano huo unafanyika siku kadhaa baada ya Trump kusema ataiongezea Canada na Mexico asilimia 25 ya ushuru wa kuingiza bidhaa nchini Marekani, hadi mataifa hayo yatakapodhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya na wahamiaji haramu wanaovuka mipaka na kuingia Marekani.

Kitisho cha Trump kimeibua mashaka nchini Canada, ambayo uchumi wake unaitegemea pakubwa Marekani na wachumi wakikiri kwamba hatua kama hiyo itauathiri uchumi wa mataifa hayo mawili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW