1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaCanada

Waziri Mkuu wa Canada kuzuru India kurekebisha uhusiano

24 Februari 2026

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney anakwenda India wiki hii akilenga kuongeza msukumo mara dufu biashara pamoja na kurekebisha mahusiano yaliyoharibika.

Canada Montreal 2026 | Waziri Mkuu Mark Carney
Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney anafanya ziara wiki hii nchini India kwa lengo la kufufua ushirikiano uliokufa tangu mwaka 2024 baina ya mataifa hayo mawiliPicha: Christinne Muschi/The Canadian Press/ZUMA/picture alliance

India ni kituo cha kwanza cha Carney kwenye ziara yake ya Asia-Pasifiki inayojumuisha pia mataifa ya Australia na Japan, akilenga kupunguza utegemezi kwa Marekani.

Carney amesema mfumo wa ulimwengu kuongozwa na Marekani unapotea taratibu na kwa maana hiyo Canada haipaswi kutegemea kwamba huenda utarejea baada ya Rais Donald Trump kuondoka.

Waziri Mkuu huyo anaondoka Alhamisi kwenda India, kwa ziara itakayofuatiliwa kwa karibu wakati yeye na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi watakapokuwa wanajaribu kurekebisha uhusiano ambao ulivunjika mwaka 2024.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW