1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Mkuu wa China kuzuru Ujerumani na Ufaransa wiki hii

15 Juni 2023

China imesema leo kuwa waziri wake mkuu Li Qiang atazitembela Ujerumani na Ufaransa kuanzia siku ya Jumapili kwa mwaliko wa kansela Olaf Scholz na serikali mjini Paris.

China | Li Qiang
Picha: GREG BAKER/AFP

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Wang Wenbin amearifu kwamba Qiang atashiriki awamu ya saba ya majadiliano ya kiserikali kati ya Ujerumani na China kabla ya kufanya ziara nchini Ufaransa kwa mazungumzo na Rais Emmanuel Macron.Xi afanya mabadiliko makubwa baraza la mawaziri

Akiwa mjini Paris, Qiang pia atahudhuria mkutano wa kilele wa kujadili njia za kupata fedha kutoka sekta ya umma na binafsi kusaidia masuala muhimu kama mapambano dhidi ya umasikini na mabadiliko ya tabianchi.

Ziara yake nchini Ujerumani imepangwa siku chache tangu serikali ya Kansela Scholz kuweka wazi nyaraka inayoitaja China kuwa dola linalotishia usalama wa kimataifa na uthabiti wa kanda ya Pasifiki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW