1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Mkuu wa China Li Qiang ziarani Jamhuri ya Ireland

17 Januari 2024

Waziri wa Mkuu wa China Li Qiang amewasili huko Jamhuri ya Ireland jana jioni kwa mazungumzo na kiongozi wa taifa hilo.

China | Li Qiang
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang Picha: Lukas Coch/AP/picture alliance

Mazungumzo hayo yatakayotuama juu ya ushirikiano wa Beijing na Umoja wa Ulaya pamoja na masuala mengine ya kimataifa na yale ya nchi hizo mbili.

Baadae leo waziri mkuu wa Ireland, Leo Varadkar, atamwandalia Li Qiang karamu ya chakula cha mchana na kisha wawili hao watafanya mazungumzo kwenye moja ya makaazi ya viongozi mjini Dublin.

Kabla ya kuanza kwa ziara ya Li, Varadkar alisema China ni nchi muhimu kisiasa na kiuchumi duniani na kwa hivyo ni muhimu kuwa na mahusiano nayo mazuri.

Li aliwasili Ireland akitokea nchini Uswisi ambako alitoa hotuba mbele ya kongamano la uchumi duniani linaloendelea mjini Davos. Aliwarai viongozi wa dunia kujiepusha na vikwazo vya kibaguzi kwenye biashara akisema ni kitisho kwa uchumi wa ulimwengu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW