Abiy afanya mazungumzo na viongozi wa Sudan
27 Januari 2023Matangazo
Kwa miaka kadhaa, Sudan na Ethiopia zimekuwa katika mzozo kuhusu mpaka na ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika Mto Nile ambalo pia limesababisha mvutano na Misri ambako pia mto huo unapita.
Soma zaidi: Bwawa kubwa la utata la Ethiopia
Ethiopia yaanza tena kujaza bwawa la Grand Renaissence
Shirika la Habari la Sudan, SUNA, limetangaza kuwa masuala kuhusu bwawa la umeme la Renaissance na mpaka yamejadiliwa katika mkutano kati ya Abiy na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel-Fattah Burhan.
Wakati wa ziara hiyo ya Jumatano (27 Januari), Abiy alikutana pia na viongozi wengine mbalimbali wa kisiasa wa Sudan ambao wengi wao wanashiriki mazungumzo ya kumaliza utawala wa kijeshi uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.