Waziri Mkuu wa Ethiopia kukutana na Rais wa Eritrea
29 Juni 2018Waziri Mkuu wa Ethiopia anatarajiwa kukutana na Rais wa Eritrea hivi karibuni, wakati viongozi wa nchi hizo mahasimu wa muda mrefu watakapokuwa wakijaribu kumaliza mzozo kati yao.
Hayo yameelezwa na kituo cha habari kinachoegemea upande wa serikali, kikimnukuu waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia. Kwa mara ya kwanza tangu nchi hizo zilipopigana vita vikali vya mwaka 1998 hadi 2000, ujumbe wa ngazi ya juu wa Eritrea uliwasili nchini Ethiopia Jumanne wiki hii katika juhudi za kusuluhisha mzozo wa mpaka ambao umeondoa kabisa mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo jirani.
Mapema mwezi huu, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, alisema yuko tayari kuheshimu maamuzi ya mahakama ya kimataifa kuhusu mpaka kati ya nchi yake na Eritrea.
Rais wa Ethiopia Isaias Afwerki amekaribisha kile alichokiita 'ishara njema' kutoka Ethiopia, na alimtuma mshauri wake Yemane Gebreab mjini Addis Ababa.