SiasaUrusi
Viktor Orban afanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin
5 Julai 2024Matangazo
Hatua ya kiongozi huyo ambaye nchi yake inashikilia uenyekiti wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya imekosolewa na viongozi wa jumuiya hiyo wakisisitiza kwamba kiongozi huyo hawakilishi mtazamo wa Umoja wa Ulaya kwenye ziara yake hiyo.
Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema kitu kitakachofunguwa njia ya kupatikana amani ya kudumu nchini Ukraine ni mshikamano na uthabiti ndani ya jumuiya hiyo ya wanachama 27.
Ziara ya Orban mjini Moscow imekuja siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO ambao utajadili mpango wa kuipatia msaada zaidi wa kijeshi Ukraine dhidi ya kile jumuiya hiyo inakiita ni uchokozi wa Urusi.