1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHungary

Orban aufananisha Umoja wa Ulaya na Umoja wa Sovieti

24 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ameufananisha Umoja wa Ulaya na uliokuwa Umoja wa Kisovieti na kuwatolea wito watu wa nchi hiyo kuupinga kama walivyoipinga Urusi mwaka 1956.

Budapest 2024 | Viktor Orban kwenye kumbukumbu ya uasi wa Hungary wa 1956
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ataka watu wake kuipinga UlayaPicha: Attila Volgyi/Xinhua/picture alliance

Waziri Mkuu Orban amesema hayo alipotoa hotuba kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Uasi wa Hungary dhidi ya uvamizi wa Wasovieti, ambao hata hivyo ulidhibitiwa vikali na wanajeshi wa Urusi.

Kribu watu 3,000 waliuliwa na 20,000 walijeruhiwa.

"Kwetu sisi, somo la 1956 ni kwamba lazima tupiganie jambo moja tu: kwa ajili ya Hungary na kwa uhuru wa Hungary," aliwaambia maelfu ya watu katika mkutano wa hadhara huko Budapest.

Orban anayefahamika kwa kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Rais Vladimir Putin wa Urusi kuliko kiongozi mwingine yoyote wa Ulaya, amekuwa akiukosoa umoja huo kutokana na kuendelea kuiunga mkono Ukraine inayopigana na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW