1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Modi apinga kurejeshwa kwa sehemu ya uhuru wa Kashmir

8 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameunga mkono uamuzi tata wa serikali yake wa mwaka 2019 kuondoa mamlaka ya ndani ya jimbo la Jammu na Kashmir.

Mmoja ya wabunge akiwa amebeba bango la kutaka mamlaka ya jimbo la Kasmir
Mmoja ya wabunge akiwa amebeba bango la kutaka mamlaka ya jimbo la KasmirPicha: Tauseef Mustafa/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameunga mkono uamuzi tata wa serikali yake wa mwaka 2019 kuondoa mamlaka ya ndani ya jimbo la Jammu na Kashmir, siku chache baada ya wabunge wapya waliochaguliwakatika eneo hilo kutaka kurejesha mamlaka hiyo.

Akitaja mmoja wa waaanzilishi wa katiba ya India, Modi alisema ni katiba ya Babasaheb Ambedkar pekee ndiyo itakayofanya kazi ndani Kashmir na kwamba hakuna mamlaka duniani inayoweza kurejesha Kifungu cha 370 kinachozungumzia sehemu huru ya Kashmir.

Modi alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa jimbo katika jimbo la magharibi la Maharashtra, anakotoka Ambedkar.

Serikali ya Chama cha Modi cha Bharatiya Janata Party (BJP) ilibatilisha mamlaka ya ndani ya Kashmir mnamo mwaka 2019 na kuligawanya jimbo hilo katika sehemu mbili zinazosimamiwa na serikali hiyo ya shirikisho, Jammu na Kashmir na Ladakh, hatua ambayo ilipingwa na makundi mengi ya kisiasa katika eneo hilo la Himalaya.