SiasaIndia
Waziri Mkuu wa India kufanya ziara nchini Ukraine
27 Julai 2024Matangazo
Hii itakuwa ziara yake ya kwanza nchini humo tangu kuanza kwa vita na wiki chache baada ya kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.
Hayo ni kulingana na vyombo vya habari nchini humo lakini Ubalozi wa Ukraine mjini New Delhi na wizara ya mambo ya nje ya India hawajatoa taarifa yoyote iliyo rasmi.
Soma pia: Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amwambia Putin kwamba vita sio suluhu
Nchi za Magharibi ziliiwekea Moscow vikwazo kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine mnamo mwaka 2022, lakini India na China zimeendelea kufanya biashara na Moscow. India inadai kutoegemea upande wowote na imekuwa ikizitaka Urusi na Ukraine kutatua mzozo wao kupitia mazungumzo na diplomasia.