1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Waziri Mkuu wa India Modi aanza ziara rasmi Marekani

22 Juni 2023

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya teknolojia na ulinzi

USA | Indiens Premierminister Modi in Washington
Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya teknolojia na ulinzi, licha ya wasiwasi wa rekodi ya haki za binaadamu nchini India.

Kwenye ziara hiyo, Biden anatarajia kuibua mashaka ya Marekani kuhusiana na kuporomoka kwa demokrasia nchini India, hii ikiwa ni kulingana na mshauri wa masuala ya usalama wa ikulu ya White House, Jake Sullivan, siku ya Jumanne.

Washington inataka kuiona India kama mshirika muhimu na mpinzani wa kimkakati dhidi ya China, wakati Modi akilenga kuimarisha ushawishi wa India, kama taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni.