1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi azuru Ukraine

23 Agosti 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi yupo nchini Ukraine kwa ajili ya ziara yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na ushirikiano katika sekta za ulinzi, sayansi na tekinolojia.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anazuru Ukraine na anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Volodymyr ZelenskyyPicha: Sergei Gapon/AFP

Waziri Mkuu Modi anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky.

Modi anafanya ziara hiyo nchini Ukraine mwezi mmoja na nusu baada ya kufanya ziara nchini Urusi.

Rais wa Ukraine alimkosoa waziri mkuu Modi kwa kufanya ziara hiyo na kumkumbatia Rais Vladimir Putin.

India imekwepa kuilaani Urusi kwa uvamizi wa nchini Ukraine na badala yake inahimiza mazungumzo na diplomasia kati ya Urusi na Ukraine ili kuutatua mgogoro kati yao.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW