1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Iraq kuanza kuondoa majeshi ya muungano

6 Januari 2024

Serikali ya Iraq jana Ijumaa ilitangaza mipango ya kuanza kuviondoa kwa nguvu vikosi vya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.

Kambi ya muungano wa kijeshi nchini Iraq
Picha inayoonyesha kambi ya jeshi ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani wanaopambana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu iliyoko jimbo la Anbar nchini Iraq. Serikali ya taifa hilo inataka kuwaondoa wanajeshi haoPicha: Ayman Henna/AFP

Hatua hiyo inafikiwa siku moja baada ya shambulizi la Marekani lililomuua kamanda wa wanamgambo wanaoiunga mkono Iran.

Ofisi ya Waziri Mkuu Mohamed al-Sudan imesema serikali inapanga tarehe ya kuunda kamati ya pamoja itakayoweka mipango ya kuviondoa moja kwa moja vikosi hivyo nchini Iraq.

Kuna wanajeshi karibu 2,500 nchini Iraq, pamoja na 900 kutoka Syria, ambao ni sehemu ya juhudi za kulizuia kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kujiimarisha.

Uamuzi wa Al Sudani unachukuliwa wakati upande wa wabunge unaoiunga mkono Iran na unaomuunga mkono waziri mkuu wakilaani vikali mauaji ya kamanda huyo Mustaq Jawad Kazim al Jawari mjini Baghdad, siku ya Alhamisi.