Waziri Mkuu wa Japan akutana na Trump mjini Washington
20 Machi 2026
Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi alipania kuthibitisha tena muungano wake na Rais Donald Trump wa Marekani siku ya Alhamisi baada ya rais huyo wiki hii kuonekana kulalamika kwamba Japan ilikuwa miongoni mwa mataifa ambayo hayakujiunga haraka na wito wake wa kusaidia kuulinda Mlango Bahari wa Hormuz.
Takaichi, ambaye alikutana na Trump katika Ikulu ya White House, alimwambia rais huyo kwamba Japan imepinga maendeleo ya Iran ya mpango wake wa nyuklia na akaunga mkono nia ya Trump ya kutaka aonekane kama kiongozi anayeleta amani, licha ya kuanzisha vita vya hiari na Iran.
Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye na Takaichi wangejadiliana katika mkutano wao kuhusu kiwango cha Japan cha uungwaji mkono kwa Marekani katika vita vya Iran, akisema wanajitahidi sana. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.