SiasaAsia
Fumio Kishida akumbuka ukoloni wa Japan kwa Korea Kusini
7 Mei 2023Matangazo
Waziri mkuu Kishida na mwenyeji wake rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini, wamesisitiza azma ya kusuluhisha mivutano ya miaka iliyopita na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zao, katika muktadha wa changamoto inayotokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Soma zaidi:Korea Kusini yathibitisha kurejesha mahusiano ya kijeshi na Japan
Waziri mkuu wa Japan amesema yeye binafsi ana machungu moyoni juu ya watu waliokabiliwa na mazingira magumu wakati wa ukoloni. Hata hivyo hakuomba radhi kwa kauli ya uwazi. Waziri mkuu huyo wa Japan ameanza ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini baada ya rais wa Korea Kusini kufanya ziara nchini Japan katikati ya mwezi wa Machi.