1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Waziri mkuu wa Japan autembelea mji wa Bucha karibu na Kiev

21 Machi 2023

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameutembelea mji wa Bucha ulioko karibu na mji mkuu wa Ukraine Kiev ambako wanajeshi wa Urusi walidaiwa kufanya mauaji ya watu wengi.

Ukraine | Japans Premierminister Fumio Kishida in Bucha
Picha: Iori Sagisawa/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa mwandishi habari wa AFP waziri mkuu huyo wa Japan aliwalisili Bucha kama sehemu ya ziara yake rasmi nchini Ukraine kabla ya kukutana kwa mazungumzo na rais Volodymyr Zelensky.

Ziara ya waziri mkuu wa Japan imesifiwa na Ukraine iliyosema ni ziara ya kihistoria, na ishara ya mshikamano na ushirikiano wa dhati kati ya nchi hizo mbili.

Soma pia: Waziri mkuu wa Japan aanza ziara ya ghafla Ukraine

Kishida ni kiongozi wa mwisho wa kundi la G7 kuitembelea Ukraine na amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka afanye ziara hiyo  katika wakati nchi yake inatajariwa kuandaa mkutano wa kilele wa kundi hilo mwezi Mei.