1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kishida hatagombea tena uwenyekiti wa chama chake

14 Agosti 2024

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema hatagombea muhula mwingine wa uwenyekiti wa chama chake katika uchaguzi ujao wa mwezi Septemba.

Japan | Fumio Kishida
Waziri Mkuu wa Japan Kishida hatagombea tena uenyekiti wa chama chakePicha: AFP

Mwenyekiti wa chama cha Liberal Democratic (LDP) ambacho kimetawala nchini Japan kwa miongo kadhaa sasa, ndiye pia anakuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Viongozi wa China waahidi msaada zaidi kuchochea uchumi

Umaarufu wa Kishida aliye na miaka 67 umeporomoka hadi kufikia chini ya asilimia 30 kutokana na kashfa iliyohusu michango ya fedha kwa ajilli ya chama chake.

Wanachama kadhaa wa chama cha Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, wamelaumiwa kwa kutoonesha wazi fedha zilizokusanywa.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW