Waziri Mkuu wa Japan yu salama baada ya kitisho cha bomu
15 Aprili 2023Matangazo
Kitu kinachoshukiwa kuwa bomu la moshi kimeripuka karibu na mahali waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida alipokuwa akifanya kampeni ya uchaguzi. Televisheni ya taifa ya Japan, NHK imeripoti kuwa kiongozi huyo ameondolewa katika eneo hilo lililo kwenye mkoa wa Wakayama bila kudhurika.
Waziri mkuu Kishida alikuwa katika eneo hilo kutoa hotuba ya kumuunga mkono mgombea wa chama chake cha kiliberali. Muda mfupi kabla ya zamu yake kuzungumza, kifaa kinachofanana na bomba kiliripuka kwa kishindo kikubwa, na mtshukiwa mmoja alikamatwa na polisi hapo hapo.
Mwaka uliopita, mtangulizi wa Fumio Kishida, Shinzo Abe alipigwa risasi na kuuawa wakati akitoa hotuba ya kampeni katika mji mkongwe wa Nara.
Vyanzo: dpa rtr afp