1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Jordan, Bisher Khasawneh ajiuzulu

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Jordan Bisher Khasawneh amewasilisha ombi la kujiuzulu Jumapili ikiwa ni siku chache baada ya uchaguzi wa bunge la nchi hiyo.

Bisher Al-Khasawneh amejiuzulu wadhifa wake kama Waziri Mkuu wa Jordan Septemba 15.09.2024
Waziri Mkuu wa Jordan, Bisher Al-KhasawnehPicha: Joseph Eid/AFP/Getty Images

Hayo ni kulingana na maafisa wenye ufahamu juu ya suala hilo. Mkuu wa Ofisi ya Mfalme Abdullah, Jaafar Hassan aliyewahi pia kuwa Waziri wa Mipango, anatarajiwa kushika nafasi ya Kasawneh. Waziri Mkuu Bisher Khasawneh, mkongwe wa diplomasia na mshauri wa zamani wa Mfalme, aliteuliwa miaka minne iliyopita.

Itakumbukwa kuwa Jumatano wiki hii, chama cha upinzani cha Kiislamu cha IAF nchini humo, ambacho ni tawi la chama cha Udugu wa Kiislamu, kilishinda viti 31 kati ya 138 katika uchaguzi wa bunge.

Soma zaidi: Chama cha Kiislamu chapata ushindi wa kihistoria uchaguzi wa bunge Jordan

Kulingana na matokeo rasmi, ushindi wa chama hicho cha Kiislamu ndiyo mkubwa zaidi tangu mwaka 1989 ambapo chama cha Udugu wa Kiislamu kilipata viti 22 kati ya 80 katika bunge la wakati huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW