SiasaKosovo
Kosovo yalaani taarifa za kukamatwa kwa maafisa wake watatu
16 Juni 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti amelaani taarifa za kukamatwa kwa maafisa wake watatu wa polisi kulikofanywa na maafisa wa Serbia. Kurti ametaja tukio hilo kama utekaji nyara na kudai kwamba lilitokea ndani ya Kosovo. Waziri Mkuu huyo amekosoa hatua ya walinda amani wa kimataifa wanaoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO waitwao KFOR, kwa kushindwa kutangaza msimamo wao kuhusiana na tukio hilo. Tukio hilo linaongeza mvutano uliopo kati ya pande hizo mbili ambao umegeuka na kusababisha machafuko katika miezi kadhaa iliyopita. Machafuko hayo yamesababisha hofu ya kuzuka tena kwa mapigano kama yaliyotokea kati ya mwaka 1998 na 99 nchini Kosovo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 10.