1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Mali aunda serikali mpya

6 Mei 2019

Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cisse ameunda serikali mpya, wiki mbili baada ya serikali ya awali kujiuzulu kutokana ongezeko la machafuko.

Mali, Bamako: Dr. Boubou Cisse (Mitte)
Picha: picture-alliance/dpa/N. Remene

Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cisse ameunda serikali mpya, wiki mbili baada ya serikali ya awali kujiuzulu kutokana ongezeko la machafuko katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Cisse amewateuwa mawaziri 37, tisa kati yao wakiwa ni wanawake, kwa mujibu wa tangazo lililosomwa jana usiku kwenye redio na televisheni za taifa.

Katika hatza ya kushangaza, Cisse amemteuwa mkuu wa shirika lililokimbwa na kashfa la UNAIDS Michel Sidibe kuiongoza wizara ya afya na maswala ya jamii nchini Mali.

Sidibe alikubali kuondoka UNAIDS mwezi Juni mwaka huu, kufuatia ripoti ya watalaamu iliyosema kuwa "uongozi wake mbovu" umelitumbukiza shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika mgogoro.

Cisse mwenyewe ataongoza wizara ya fedha kando na kuwa waziri mkuu, wakati viongozi wa upinzani Tiebile Drame na Amadou Thiam wameteuliwa kusimamia wizara za mambo ya kigeni na mageuzi ya kitaasisi.