1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNew Zealand

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda atangaza kujiuzulu

19 Januari 2023

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ametangaza kwamba ataachia ngazi kama kiongozi wa nchi hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao wa Februari

Neuseeland Premierministerin Jacinda Ardern kündigt Rücktritt an | ARCHIV
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

 Ardern ametangaza kwamba hatogombea tena nafasi hiyo. Ardern ametoa tangazo hilo lililowashtua wengi akisema hana nguvu tena za kuiongoza nchi hiyo. Waziri huyo mkuu amesema aliyekuwa akijizuia kububujikwa na machozi wakati alipokuwa akitangazo hayo, amesema kimekuwa kipindi kigumu cha miaka mitano na nusu na kwamba yeye ni binadamu wa kawaida tu na alihitaji kujiuzulu.

Ardern asema anaamini hawawezi kushinda

Ardern amesema kuwa anaamini kwamba hawawezi kushinda uchanguzi, lakini kwasababu anaamini wanaweza na watashinda na wanahitaji mtu mwengine kwa ajili ya changamoto hiyo.

Kura ya kumchagua kiongozi mpya wa chama tawala cha Leba itafanyika Jumapili na atakayechaguliwa atakuwa waziri mkuu hadi uchaguzi mkuu ujao utakapofanyika mnamo Oktoba 14.