1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAZIRI MKUU WA POLAND AJERUHIWA:

5 Desemba 2003

WARSAW: Waziri mkuu wa Poland Leszek Miller amejeruhiwa baada ya helikopta ya serikali kulazimika kutua kwa dharura.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali,waziri mkuu Miller na watu wengine saba wamepelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa katika ajali hiyo.Yadhaniwa kuwa hitilafu kwenye injini ya helikopta ndio imesababisha ajali,aliongezea msemaji wa serikali.Kwa upande mwingine madaktari wamearifu kuwa waziri mkuu Miller ameumia kwenye uti wa mgongo na huenda akabakia hospitali kwa muda wa juma moja.