1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Poland apewa jukumu la kuunda serikali

7 Novemba 2023

Rais wa Poland Andrej Duda amempa waziri mkuu wa sasa Mateusz Morawiecki, jukumu la kuunda serikali mpya, baada ya chama tawala cha kihafidhina cha PiS kushinda viti vingi katika uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

Rais wa Poland Andrzej Duda na Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki
Rais wa Poland Andrzej Duda na Waziri Mkuu Mateusz MorawieckiPicha: JANEK SKARZYNSKI/AFP

Hata hivyo Chama cha PiS kilishindwa kupata wingi wa viti bungeni, na hivyo kuwa na nafasi ndogo ya kuunda serikali ya mseto.

Uamuzi wa rais Duda ambaye ni mshiriki wa serikali ya sasa, unatazamiwa kuchelewesha uundwaji wa serikali nchini Poland.

Wanasiasa wa upinzani wamekosoa uamuzi huo wakisema unazusha mashaka ya kisiasa na kuchelewesha uundwaji usioepukika wa serikali chini ya kiongozi wa upinzani na rais wa zamani wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW