1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sonko akosoa mashambulizi kwa wafuasi wake

12 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko ametaka ulipaji kisasi kufuatia kile alichokielezea kama mashambulizi dhidi ya wafuasi wa chama chake cha Pastef.

Senegal Dakar | Finanzlage | Pressekonferenz von Ousmane Sonko
Picha: SEYLLOU/AFP

Sonko, ambaye amekuwa mkuu wa serikali tangu ilipoingia madarakani mwezi Aprili, alizungumzia ghasia zilizotokea katika mji mkuu wa Dakar, na miji mingine miwili.

Aidha kiongozi huyo, amewashutumu wafuasi wa Meya wa Dakar Barthelemy Dias anayeongoza muungano pinzani wa Samm Sa Kaddu kwa kuwashambulia wafuasi wa chama chake.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye atangaza kulivunja bunge

Muungano huo nao umesema Sonko anawajibika kwa lolote litakalowatokea wanachama wake, wanaharakati, wafuasi na wapiga kura. Senegal inatarajia kufanya uchaguzi wa bunge jipya siku ya Jumapili, baada ya rais Bassirou Diomaye Faye kuvunja bunge lililokuwa likidhibitiwa na upinzani.