SiasaSlovakia
Waziri Mkuu wa Slovakia afanyiwa upasuaji mwingine
18 Mei 2024Matangazo
Maafisa wanasema baada ya upasuaji huo, hali ya mwanasiasa huyo bado si ya kuridhisha.
Serikali mjini Bratislava imesema taarifa zaidi juu ya hali ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico itawekwa wazi "wakati hali itakaporuhusu." Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemuandikia barua rais wa Slovakia Zuzana Caputová, na kulaani kitendo hicho huku akimtakia ahueni kiongozi huyo.
Mshukiwa wa tukio hilo ambaye inasemekana ni mzee mwenye umri wa miaka 71 anashikiliwa na Polisi. Hata hivyo waendesha mashitaka wamezitaka mamlaka za usalama kutotoa maelezo zaidi kuhusu kesi hiyo.