MigogoroSudan
Waziri Mkuu wa Sudan ataka UM uunge mkono mpango wa amani
23 Desemba 2025
Matangazo
Akizungumza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Idris amesema mpango wa usitishaji vita unahitajika haraka iwezekanvyo chini ya usimamizi wa Umoja huo, ule wa Afrika na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Amesisitiza mpango huo ni sharti uwalazimishe wanamgambo wa RSF kuondoka kwenye maeneo wanayoyashikilia na kisha kuruhusu kuundwa serikali ya mpito itakayoandaa uchaguzi huru nchini Sudan.
Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Jeshi la Sudan linapambana na vikosi vya wanamgambo wa RSF katika mzozo ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni kukimbia miji yao.