SiasaThailand
Waziri Mkuu wa Thailand atangaza uchaguzi mkuu kufanyika Mei
21 Februari 2023Matangazo
Chan-O-Cha ambaye yeye mwenyewe anawania uchaguzi huo licha ya ukosoaji unaoandama utawala wake, amesema atalivunja bunge mnamo mwezi Machi ili kufungua njia ya uchaguzi kufanyika mwezi Mei.
Katika wakati uchumi wa Thailand umeterereka na sekta muhimu ya utalii imeathiriwa na janga la corona, uchaguzi huo utakuwa kipimo kwa utawala wa Chan-O-Cha ambaye umaarufu wake umeporomoka.
Kiongozi huyo atatetea kiti chake kupitia chama kipya alichokiunda cha Ruam Thai Sang baada ya chama tawala kusema kitampendekeza mwanasiasa mwengine kuwania kiti cha waziri mkuu.