SiasaUfaransa
Waziri mkuu wa Ufaransa akemea uhalifu wa waandamanaji
24 Machi 2023Matangazo
Hali inazidi kuwa tete katika baadhi ya miji nchini humo. Borne ameandika kupitia ukurasa wa twitter akisema wana haki kuandamana na kuwasilisha madai yao lakini akaonya kwamba vurugu na uharibifu ulioshuhudiwa jana havikubaliki.
Soma pia: Maandamano yaendelea Ufaransa kupinga mpango wa mageuzi ya pensheni
Waziri wa mambo ya ndani Gerald Darmanin amesema zaidi ya askari 150 wa vikosi vya usalama wamejeruhiwa na zaidi ya watu 170 wamekamatwa. Kulingana na wizara hiyo zaidi ya watu milioni 1 waliandamana ingawa taarifa nyingine zinasema karibu watu milioni 3.5 walishiriki maandamano hayo.