SiasaUholanzi
Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amejiuzulu
8 Julai 2023Matangazo
Kiongozi huyo wa muda mrefu zaidi wa Uholanzi na mmoja wa wanasiasa wenye uzoefu zaidi barani Ulaya, amesema baada ya siku kadhaa za mazungumzo kuhusu mgogoro huo kati ya vyama vinne, wameshindwa kufikia makubaliano.
Mpasuko huo unajiri kufuatia mpango ya Rutte wa kuweka vizuizi vya kuziunganisha tena familia za wanaotafuta hifadhi.
Soma pia: Merkel na Rutte wajadili mageuzi ya Ulaya
Baada ya waziri mkuu huyo kujiuzulu, tume ya uchaguzi ya Uholanzi imesema uchaguzi wa mapema zaidi unaweza kuandaliwa katikati ya Novemba, huku Rutte akisema ataingoza serikali ya muda hadi wakati huo.