Waziri Mkuu wa Uingereza aanza rasmi ziara yake China
28 Januari 2026
Ameyasema hayo mbele ya viongozi 50 wa kibiashara walioambatana naye katika safari hiyo. Ziara ya Starmer China inaashiria juhudi za Uingereza za kutaka kushirikiana na taifa hilo katika masuala ya diplomasia na uchumi baada ya mivutano ya muda mrefu.
Mizozo ya HongKong, Ukraine na Urusi ilikwamisha ushirikiano
Mivutano iliyozorotesha ushirikiano wa nchi hizo ni pamoja na ukandamizaji unaofanywa na China dhidi ya uhuru wa kisiasa wa Hong Kong na hatua ya China kuiunga mkono Urusi katika vita dhidi ya Ukraine.
Hivi karibuni Waziri Mkuu huyo wa Uingeraza hata hivyo alikataa kujibu kama ataitumia ziara hii kuiomba China iishinikize Urusi kusitisha vita dhidi ya Ukraine. China inatazamia kuitumia ziara ya Starmer kama nafasi ya kujinasibu kuwa mshirika wa kuaminika badala ya Marekani ambayo kwa sasa haitabiriki.