1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak amfuta kazi Braveman kufuatia ukosoaji wake wa polisi

13 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amemfukuza Waziri wake wa Mambo ya Ndani Suella Braveman, kufuatia ukosoaji wake dhidi ya polisi na namna walivyowadhibiti waandamanaji waliokuwa wakiwaunga mkono Wapalestina.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa pamoja na Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella Braverman
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa pamoja na Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella BravermanPicha: Phil Noble/empics/picture alliance

Duru za Serikali zimesema Braveman alikubali kuachia wadhifa huo baada ya Sunak kumuomba kufanya hivyo. Hata hivyo, Sunak amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa wabunge wa upinzani na wa chama tawala cha Conservative waliomtaka kumuondoa waziri huyo.

Maelfu ya waandamanaji wanayoiunga mkono Palestina waandamana katika miji mbali mbali duniani

Mhariri wa masuala ya siasa kwenye gazeti la Sun amesema pengine nafasi yake itachukuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje James Clevery, wakati Sunak akifanya mabadiliko ya baraza lake. 

Aidha, Waziri Mkuu wa zamani David Cameron huenda akarejea serikalini baada ya kuonekana hii leo akielekea ofisi za Waziri Mkuu zilizoko Downing Street.