1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rishi Sunak kukutana na Kansela Scholz nchini Ujerumani

24 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak atakutana leo Jumatano na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.

 Kansela Olaf Scholz akisalimiana na  Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akisalimiana na Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Anna Szilagyi/Getty Images

Ziara hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na inatazamiwa kuimarisha ushirikiano wa usalama baada ya London kutangaza hatua ya kuongeza matumizi ya ulinzi.

Kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya Uingereza,  viongozi hao wawili wanatarajiwa kutangaza mipango ya ushirikiano wa kijeshi kwa kuendeleza udhibiti wa mifumo ya makombora na pia kujadili kuhusu masuala ya uwekezaji na miradi ya nishati.

Sunak ambaye alikuwa hajafanya ziara rasmi nchini Ujerumani tangu aliposhikilia wadhifa wa Waziri Mkuu wa Uingereza mnamo Oktoba mwaka 2022, alipunguza safari zake za kimataifa na kukabidhi sehemu kubwa ya majukumu ya kidiplomasia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje David Cameron.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW