1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Ukraine akutana na waziri wa jeshi la Marekan

20 Novemba 2025

Waziri Mkuu wa Ukraine, Yulia Svyrydenko, Alhamisi amekutana na Waziri anayesimamia Jeshi la Marekani, Daniel Driscoll, mjini Kiev.

Ternopil, Ukraine 2025
Jengo la makaazi lililoharibiwa kwa shambulizi la Urusi huko Ternopil, UkrainePicha: Thomas Peter/REUTERS

Yulia ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake katika jukwaa la mtandao wa kijamii.

Amesema ziara hiyo inatoa fursa muhimu kwa maafisa wakuu wa jeshi wanaoongozana na waziri huyo kutathmini hali ilivyo Ukraine na kushuhudia moja kwa moja matokeo ya uchokozi wa Urusi.

Jana, Driscoll na ujumbe wa maafisa wakuu wa kijeshi wa Marekani, alikutana na mkuu wa jeshi la Ukraine.

Ukraine yapokea miili ya wanajeshi

Wakati huo huo, Ukraine imeipokea miili 1,000 ya kile ambacho Urusi imesema ni askari wake waliouawa.

Kituo cha kuratibu masuala ya wafungwa wa kivita cha Kiev, kimesema leo kuwa wachunguzi kutoka vyombo vya sheria, na mashirika ya kitaalamu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, hivi karibuni watafanya uchunguzi wote muhimu na kuitambua miili hiyo iliyorejeshwa nyumbani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW