Waziri mkuu wa Uturuki ziarani mjini Washington
6 Novemba 2007Waachiwe wawahujumu waasi wa kikurd wa PKK au vipi?Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitaraji kupata risdhaa ya Marekani jana alipokutana na rais George W. Bush mjini Washington.Yeye ndie mwenye kuwaamuru wanajeshi wanaoongozwa na Marekani,na wenye kudhibiti hali ya mambo nchini Irak.Lakini licha ya matamshi bayana dhidi ya PKK,rais Bush hakutoa ridhaa kwa wanajeshi wa Uturuki kulivamia eneo la kaskazini la Irak.
Waziri mkuu wa Uturuki alisema hata kabla ya mkutano huo,anasubiri “hatua muhimu “za Marekani kuelekea waasi wa PKK-George W.Bush hakumvunja moyo mgeni wake.Amemridhisha Erdogan.Waziri mkuu wa Uturuki alisikia kile alichotaka kukisikia.George W. Bush alisema:
“PKK ni kundi la kigaidi.Ni adui wa Uturuki,adui wa Irak na audi wa Marekani.”
Bush hakuishia hapo.Seuze tena la muhimu lilikua kuzuwia kitisho cha Uturuki cha kuvamia eneo la kaskazini mwa Irak,ambako PKK wamepiga kambi zao.Rais wa Marekani amependekeza mpango madhubuti wa ushirikiano na baada ya mazungumzo yao aliufafanua mpango huo akisema:
“Tumezungumzia jinsi ya kushirikiana na jinsi ya kujihami dhidi ya PKK.Tumekubalian kwamba,ni muhimu kubadilishana habari zinazokusanywa na idara za upelelezi.Na tumesema ni muhimu kwa wanajeshi wetu kuendeleza maingiliano ya mara kwa mara.”
Hakuna,si rais Bush na wala si mgeni wake waziri mkuu wa Uturuki Erdogan aliyefafanua ni ushirikiano wa aina gani wa kijeshi na idara za upelelezi wanaokusudia.Katika mkutano wa baadae pamoja na waandishi habari waziri mkuu wa Uturuki Racep Tayyib Erdogan amesema tuu “wanakubaliana ,watu wasitegemee kwamba atasimulia yote waliyoyazungumza.”Ameongeza kusema,ameridhika na matokeo ya mazungumzo yao.Matamshi hayo yanazusha eti eti.
La bayana ni kwamba Marekani imeitaka serikali ya Irak iwajibike pia na kushirikiana nao katika kuwavunja nguvu wanamgambo wa PKK.
Rais Bush amesisitiza umuhimu wa kushirikiana,hakupendelea lakini kusema mengi alipoulizwa na waandishi habari kuhusu uwezekano wa Uturuki wa kulivamia eneo la kaskazini la Irak.