1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Waziri mkuu wa zamani wa Burundi, Bunyoni akamatwa

23 Aprili 2023

Mamlaka nchini Burundi zimemkamata waziri mkuu wa zamani, Alain-Guillaume Bunyoni, ikiwa ni miezi saba tangu alipoondolewa madarakani.

Kongo | Besuch Präsident Burundi Evariste Ndayishimiye
Picha: Giscard Kusema

Taarifa hii ni kulingana na tume ya haki za binaadamu nchini humo na chanzo cha ngazi za juu cha usalama, jana Jumamosi.

Bunyoni aliyekamatwa usiku wa kuamkia kumbukumbu ya miaka 51 ya kuzaliwa kwake, alikuwa waziri mkuu kati ya 2020 hadi Septemba 2022, lakini alifutwa kazi katika mabadiliko makubwa baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuchukua madaraka mnamo 2020, kufuatia kifo cha ghafla cha rais Pierre Nkurunziza.

Duru za usalama zilisema siku ya Jumatatu, polisi na maafisa wake walipekua nyumba zake tatu lakini hawakumkuta na siku ya Jumatano, waziri wa mambo ya ndani Martin Niteretse aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiongozi huyo wa zamani anatafutwa.

Soma Zaidi: Burundi yafanya msako wa Waziri Mkuu wa zamani Bunyoni aliyetoweka

Ingawa jumuiya ya kimataifa inaona mabadiliko ndani ya taifa hilo tangu Ndayishimiye alipochukua mamlaka, lakini Kamati ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2021 ilisema hali ya haki nchini Burundi ni mbaya.