Waziri Mkuu wa zamani wa Canada akiri kapokea hela lakini asema sio murungura
14 Desemba 2007Waziri mkuu wa zamani wa Canada, Brian Mulroney, amekanusha madai kuwa alipokea rushwa alipokuwa ofisini mwaka wa 1988.Inadaiwa kuwa murungura aliula kutoka kwa mfanya biashara ya silaha wa Ujerumani. Lakini akiwa mbele ya kamati ya kibunge mjini Ottawa Canada- amekiri kuchukua dola za Kanda zaidi ya laki mbili kutoka kwa Karlheinz Schreiber baada ya kuondoka ofisini mwaka wa 1993.Mulroney asema hilo lilikuwa kosa.
Mjerumani Schreiber anatakiwa Ujerumani kwa madai kadhaa mkiwemo kukwepa kulipa kodi,ufisadi pamoja na udanganyifu.Waongoza mashataka wa Ujeruamni wanaamini kuwa raia huyo ni mhusika mkuu katika kashfa ya kufadhili chama, ambapo chama cha Christian democtratic Party –CDU- cha Kansela wa zamani wa Ujerumani-Helmut Kohl, kilihusishwa.