1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Waziri Mkuu wa zamani wa China Li Keqiang amefariki dunia

27 Oktoba 2023

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang, amefariki dunia mapema leo mjini Shanghai akiwa na umri wa miaka 68.

Aliekuwa Waziri Mkuu wa China Li Keqiang
Aliekuwa Waziri Mkuu wa China Li KeqiangPicha: Wang Zhao/Pool/Getty Images

Taarifa ya shirika la habari la nchini humo limesema Keqiang amekutwa na umauti baada ya kupatwa ghafla na shambulio la moyo.

Kulingana na taaarifa hiyo, waziri mkuu huyo wa zamani alianzakuugua Alhamisi na alikufa baada ya juhudi za kuokoa maisha yake kugonga mwamba.

Li Keqiang alijiuzulu wadhifa wake Machi 10 baada ya kuwa miaka 10 madarakani chini ya utawala wa Rais  Xi Jinping. Kwa miaka mingi kumekuwa na uvumi kuhusu afya ya Keqiang.

Soma pia:Keqiang amekuwa mmoja ya viongozi wa China waliosifika kwa kukubali mageuzi kwa haraka tofauti na viongozi wengi nchini humo

Baadhi ya wanadiplomasia waliwahi kusema katika mazungumzo ya faragha kuwa, wakati wa ziara zake nje ya China ratiba za Li Keqiang zilitawaliwa na vipindi virefu vya mapumziko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW