1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia

15 Oktoba 2025

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo nchini India.

Nairobi 2022 | Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia nchini India akiwa na umri wa miaka 80Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Hospitali ya Devamatha katika jimbo la Kerala imethibitisha taarifa za kifo chake hivi leo. Odinga ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 80, aliwahi kugombea urais wa Kenya mara tano katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu. 

Mwezi machi,  Raila Odinga  alikuwa amesaini makubaliano ya kisiasa na rais wa sasa William Ruto ambayo yalikiruhusu chama chake cha upinzani cha ODM kushiriki katika mchakato muhimu wa kupitisha sera huku baadhi ya wanachama wake wakiteuliwa kuwa mawaziri.

Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa na kukitangaza rasmi kifo cha Odinga. Viongozi mbalimbali duniani wameanza kutuma salamu zao za rambirambi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW