1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Nepal akamatwa na polisi

28 Machi 2026

Waziri Mkuu wa zamani wa Nepal Sharma Oli na aliyekuwa Waziri wake wa mambo ya ndani Ramesh Lekhak wamekamatwa na polisi mapema Jumamosi kutokana na uhusika wao katika vifo vya raia kwenye maandamano ya Septemba, 2025.

Waziri Mkuu wa zamani wa Nepal Sharma Oli anashikiliwa na polisi kuchunguza uhusika wake katika maandamano ya Septemba 2025 yaliyosababisha vifo vya raia.
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Nepal K.P. Sharma OliPicha: Sabrina Dangol/REUTERS

Msemaji wa polisi wa Kathmandu, Om Adhikari amesema mamlaka zimechukua hatua hiyo ili kuchunguza jukumu la mawaziri hao wa zamani katika maandamano ya kupinga ufisadi yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka jana na yaliyosababisha vifo vya zaidi ya raia 70.

Jopo la serikali lapigilia msumari kukamatwa Oli na Lekhak

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya jopo lililoteuliwa na serikali kupendekeza wawili hao washtakiwe kwa tuhuma za uzembe katika kuyasimamia maandamano hayo.

Oli na Lekhak wamekamatwa siku moja baada ya Waziri Mkuu mpya Balendra Shah kuapishwa. Maandamano katika taifa hilo la Kusini mwa Asia yaliyofanyika mwaka uliopita yaliyoongozwa na vijana maarufu kama Gen Z yaliuangusha utawala wa Oli na yalichochewa na hatua ya serikali kupiga marufuku mitandao ya kijamii.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW