1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Nawaz Sharif arejea Pakistan baada ya miaka minne uhamishoni

21 Oktoba 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif amerejea nchini humo leo kwa kutumia ndege maalumu akitoka Dubai, hatua inayokamilisha kipindi cha miaka minne alichokaa uhamishoni mjini London nchini Uingereza

Wafuasi wa Nawaz Sharif wacheza ngoma za kitamaduni wanapowasili kwa mkutano wa kumkaribisha nyumbani mjini Lahore Oktoba 21, 2023
Wafuasi wa Nawaz Sharif wacheza ngoma za kitamaduni wanapowasili kwa mkutano wa kumkaribisha nyumbani mjini LahorePicha: K.M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Sharif anarejea nyumbani kuelekea uchaguzi mkuu katika taifa hilo unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwakani, ambapo anatafuta kupata uungwaji mkono wa wapiga kura. Akiwahutubia waandishi wa habari kabla ya kuondoka Dubai kuelekea Islamabad, Sharif amesema kuwa leo anaelekea Pakistan baada ya miaka minne na anaona raha sana kwa neema ya mwenyezi Mungu.

Soma pia: Pakistan yamruhusu Sharif kurejea nyumbani kutoka uhamishoni

Sharif ameonPakistan yamruhusu Sharif kurejea nyumbani kutoka uhamishonigeza kuwa anatamani hali nchini Pakistan ingekuwa imeimarika wakati alipokuwa uhamishoni alipokimbilia mnamo mwaka 2019 miaka miwili baada ya kujiuzulu wadhifa wa waziri mkuu baada ya kutiwa hatiani kwenye kesi ya ufisadi. Sharif atasafiri kuelekea mji mkubwa wa Mashariki wa Lahore, ambapo wafuasi wake tayari wamekusanyika kwa ajili ya mkutano wa kumkaribisha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW