1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mpya wa nje wa Syria aanza ziara ya kwanza UAE

6 Januari 2025

Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Syria Asaad al-Shaibani amewasili leo katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Ni ziara yake ya kwanza nchini humo tangu waasi walipomuondoa madarakani rais Bashar al-Assad mwezi uliopita.

Syrien Damaskus 2025 |  Neujahrsfeier nach Sturz von Assad-Regime
Watu waksherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya kwenye Uwanja wa Umayyad mjini Damascus, Syria, Jumanne, Desemba 31, 2024.Picha: Leo Correa/AP/picture alliance

Shirika la habari la serikali SANA limesema Shabaini aliandamana na waziri wa ulinzi Murhaf Abu Qasra na mkuu wa idara ya intelijensia Anas Khattab. Ziara yao katika Umoja wa Falme za Kiarabu inajiri baada ya kuwatembelea majirani zao wa eneo la Ghuba Qatar jana Jumapili na Saudi Arabia wiki iliyopita. Wachambuzi wanasema Umoja wa Falme za Kiarabu una mashaka makubwa na viongozi hao wapya wa Syria ukionyesha kutokuwa na imani na siasa za kiislamu na hofu ya ushawishi mkubwa wa Uturuki katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita. Qatar na Uturuki, ambazo ziliuunga mkono upinzani uliompinga Assad, zilizifungua balozi zake mjini Damascus baada ya Assad kukimbilia Moscow, Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW