Belousov: Kipaumbele ni kupata ushindi dhidi ya Ukraine
15 Mei 2024Belousov ameliambia bunge la Urusi kuwa, lengo lao kuu linasalia kuhakikisha malengo ya kijeshi na kisiasa ya oparesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine inatimizwa.
Belousov ameongeza kuwa Urusi haina nia ya kuhamasisha upya vijana kujiunga na jeshi ama kuchukua hatua za dharura ili kuongeza idadi ya wanajeshi wake.
Ni nadra sana kwa Urusi kuzungumzia juu ya hasara iliyopata katika mzozo huo na Ukraine.
Soma pia: Hujuma za Urusi zaendelea kuutikisa mji wa Kharkiv, Ukraine
Mara ya mwisho kwa Moscow kutoa takwimu rasmi ilikuwa mnamo Septemba mwaka 2022 ambapo ilisema wanajeshi wake 5,937 waliuawa katika mapigano.
Rais Vladimir Putin mnamo siku ya Jumapili alimteua mchumi Andrei Belousov kuchukua nafasi ya Sergei Shoigu kama waziri wa ulinzi, hatua ya kushangaza baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita nchini Ukraine.